9 Oktoba 2023 - 19:10
Ebrahim Raisi: Tufani ya al-Aqswa ni matokeo ya mrundikano wa dhulma za Wazayuni dhidi ya Wapalestina

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ujumbe wake kwa taifa lenye fahari la Palestina amepongeza harakati iliyoweka historia ya mhimili wa muqawama na kusisitiza kuwa, Tufani ya Al-Aqswa ni matokeo ya mrundikano wa dhulma na uonevu unaofanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Iranpress, katika ujumbe wake Seyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya Iran, ameeleza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inawaalika walimwengu wote kutazama ukweli wa jinsi mrundikano wa dhulma na uonevu dhidi ya taifa lililokandamizwa la Palestina, kuendelea kuwatusi na kuwatukana wanawake na wafungwa na kukivunjia heshima kibla cha kwanza cha Waislamu kkwamba, sio mambo ambayo yatadumu milele bali yaatakabiliwa na muqawaama wa mataifa.

Huku akisisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaunga mkono kujihami kihalali kwa taifa la Palestina, Ebrahim Raisi amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel na waungaji mkono wake wanabeba dhima ya uhatarishaji usalama wa mataifa ya eneo hili ambapo wanapaswa kutoa majibu ya hili.Katika sehemu nyingine ya ujumbe wake, Rais wa Iran amekosoa vikali hatua ya baadhi ya mataifa ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na kufanya mapatano na utawala huo ghasibu na ameyataka mataifa ya Kiislamu na umma wote wa Kiislamu kuingia uwanjani na kuwaunga mkono kwa dhati wananchi wa Palestina. Rais amesifu na kuzipongeza kambi za muqawama kuanzia Palestina, Lebanon, Syria, Iraq, Afghanistan na Yemen pamoja na viongozi na mashahidi wa muqawama hususan Shahidi Qassim Suleimani na amewahutubu Wazayuni kwa kusisitiza kwamba, mahesabu yamebadilika, kupenda vita ni kwa madhara ya Wazayuni na taifa la Palestina ndilo litakaloibuka na ushhindi katika medani ya vita.

342/